Jumapili 30 Agosti 2026 - 13:18
“Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu” Yaadhimisha Kumbukumbu ya Kuuwawa Hujaatul-Islam Sayyid Abbas al-Mousawi kwa Kufanya Mkutano Kuhusu “Mtazamo wa Qur’ani katika Fikra Zake”

Hawza/ “Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu ya Lebanon” imeadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya kuuwawa Hujaatul-Islam Sayyid Abbas Ali al-Mousawi kwa kuendesha kikao kilikuwa na anuani “Mtazamo wa Qur’ani katika Fikra za Hujaatul-Islam al-Mousawi.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, “Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu ya Lebanon” imeadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya kifo cha Sayyid Abbas Ali al-Mousawi kwa kuendesha kikao kilichoitwa “Mtazamo wa Qur’ani katika Fikra za Hujaatul-Islam Sayyid Abbas Ali al-Mousawi (ra).”

Sheikh Malas: Sayyid al-Mousawi alikuwa mwenye juhudi kubwa katika nyanja ya kielimu, na makumi ya vitabu na maandishi kuhusu Uislamu na Ahlul-Bayt (as) yamechapishwa kutoka kwake

Msimamizi wa kikao hiki alikuwa mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Mustafa Malas, ambaye alisema: “Kufahamiana na Sayyid Abbas al-Mousawi (ra) kulianza takribani miaka arobaini iliyopita. Alikuwa mwenye juhudi kubwa katika nyanja ya kielimu, na makumi ya maandishi na vitabu kuhusu Uislamu, maarifa yake, Ahlul-Bayt (as), pamoja na uwanja wa tafsiri ya Qur’ani Tukufu na urithi wa Maimamu (as), vimechapishwa kutoka kwake. Alidumu katika kutekeleza majukumu yote aliyoyabeba au aliyokabidhiwa, kuanzia katika kuhubiri na kuongoza, kufanya utafiti na kuandika vitabu, hadi shughuli za kijamii na za kiutawala.”

Sheikh Khazem: Uzoefu wa Sayyid al-Mousawi unaweza kuangaliwa kama juhudi za kuirejesha Qur’ani kuwa kitovu cha mchakato wa tafsiri

Kwa upande wake, mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Jumuiya hiyo, Sheikh Ali Khazem, alisema: “Ni jambo gani linalomtofautisha Sayyid Abbas al-Mousawi kama mfasiri? Je, alikuwa na mkusanyiko tu wa rai za kitafsiri, au nyuma ya rai hizo kulikuwa na mtazamo ambao ungeweza kujengwa upya? Utafiti huu umefikia hitimisho kwamba sifa ya pekee ya Sayyid al-Mousawi haikuwa katika kanuni moja ya kitafsiri, bali katika mbinu ambayo kupitia hiyo aliunganisha baina ya kuhifadhi Qur’ani na kuifanya kuwa rejea, kuweka nidhamu katika uelewa wake, na kisha kuamilisha maana zake katika uongofu na urekebishaji.”

Aliongeza: “Utafiti huu uliangazia mtazamo uliotawala uelewa wake wa Qur’ani na tafsiri yake, na namna alivyohama kutoka katika misingi ya uelewa kwenda katika ujenzi wa maana, na kisha kutoka katika maana kwenda katika uongofu na urekebishaji; ambao ni mtazamo wa kimapinduzi na unaoendelea hatua kwa hatua. Kwa kuzingatia matokeo ya utafiti huu, uzoefu wa Sayyid al-Mousawi unaweza kuangaliwa kama juhudi za kuirejesha Qur’ani kuwa kitovu cha mchakato wa tafsiri, bila kuitenganisha na mwanadamu na uhalisia.”

“Mtazamo wake uliunganisha baina ya kusisitiza nidhamu ya maana, uhalali wa dhahiri ya matini na kuifanya Qur’ani kuwa kipimo, pamoja na juhudi za kurejesha ufanisi wa matini katika kuunda uelewa, uongofu na harakati. Umuhimu wa mtazamo wake wa kiutambuzi umo katika muunganiko huu: Qur’ani iliyohifadhiwa ambayo haiathiriwi na matamanio ya nafsi; maana yenye nidhamu ambayo haifungwi na historia; na uongofu ambao hautenganishwi na uhalisia. Utatu huu, kwa mujibu wa uchambuzi wa utafiti huu, ndilo jambo mashuhuri zaidi linaloupa uzoefu wake wa kitafsiri umoja na sifa yake ya pekee.”

Sheikh Haninah: Tumefanikisha mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Umma wetu katika miaka mia moja iliyopita, nayo ni kuvunja nguvu za adui Mzayuni na adui wa Kimarekani

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Jumuiya hiyo, Sheikh Ghazi Haninah, alisema: “Kile ambacho Muqawama umeweza kukipata katika kipindi cha miaka mitatu ya mapambano yetu dhidi ya adui Mzayuni, hususan vita vilivyoanza kwa Operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa, na baadaye kudhihirika katika vita vyote ambavyo Muqawama umepitia kusini mwa Lebanon, pamoja na yale ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeyatoa, yale ambayo waarabu na Waislamu wa Yemen wameyatoa katika ardhi ya Yemen, na yale ambayo watu jasiri na mashujaa wa Iraq wameyatoa; kupitia hayo tumefanikisha mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Umma wetu katika miaka mia moja iliyopita, nayo ni kuvunja nguvu za adui Mzayuni na kuvunja nguvu za adui wa Kimarekani.”

“Wakati Sayyid, Kiongozi Shahidi, Sayyid Ali Khamenei (ra), alipokuwa akizungumza na kusema kwamba Marekani lazima iondoke Asia Magharibi, tuliiondoa Marekani kutoka Asia Magharibi na tukasajili ushindi ambao hadi sasa bado tunalipa gharama ya kuutetea mbele ya adui Mzayuni.”

Aliongeza: “Kwa hiyo, leo mtazamo ambao Sayyid Abbas al-Mousawi aliufuata ndio uleule mfumo wa mtazamo wa wanazuoni wa Kiislamu ambao sisi leo tunasimama juu yake. Kwa baraka za Mwenyezi Mungu aliyetukuka, na chini ya uongozi wenye hekima wa Sayyid Kiongozi, Imam Mujtaba Khamenei (Mwenyezi Mungu amhifadhi), na chini ya uongozi wa Hujaatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah, tunaendelea mbele ili ahadi ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Utukufu, itimie; kurejea Palestina katika ardhi yake, kurejea watu wa Palestina katika nchi yao, na kurejea watu wa kusini ndani ys kusini kwa hali ya kuwa washindi, hata kama itachukua muda gani.”

Kwa upande mwengine, Hujaatul-Islam Sheikh Hassan Abdullah, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jumuiya hiyo, alisema: “Maneno yoyote nitakayoyapata hayatatosheleza kumpa haki yake mwanamume huyu mkubwa. Mimi ni miongoni mwa wanafunzi wake, na nilisoma kwake zaidi ya kitabu cha Al-Lum‘ah ad-Dimashqiyyah. Alikuwa na mtindo wa pekee, si katika kufafanua tu ibara, bali pia katika kuzama ndani ya maudhui ya ibara hizo ili kufikia misingi ya awali ambayo mtafiti au mwandishi alianza nayo ili kufikia hitimisho alilolifikia. Kwa hiyo, nilinufaika sana na elimu yake, na kwa maneno haya machache ambayo sina uwezo nayo, sitaweza kumpa haki yake.”

Aliongeza: “Katika kipindi chote nilichokuwa pamoja naye, mwishoni mwa miaka ya sabini, nilihisi kwamba alikuwa akinifuatilia bila kulitamka hilo kwa ulimi wake; yaani, daima alikuwa akitoa nasaha kwa namna ambayo kana kwamba anasema: ‘Unaonaje?’ Badala ya kutoa nasaha moja kwa moja na kusema: ‘Unaonaje kuhusu jambo hili na lile?’ Kwa hiyo, nilikuwa nikielewa kwamba rai hiyo ilikuwa ni rai yake na kwamba alitaka kuielekeza kwa ishara. Na katika mambo mengi nilikuwa nikijitahidi kutekeleza nasaha hizo.”

Sheikh Abdullah alieleza: “Alibeba kwa kiwango kikubwa sana dhamira ya Muqawama, na daima alikuwa akiulizia kwa undani mambo yanayohusiana na Muqawama. Kuna misimamo mingi iliyokuwepo pamoja na Sayyid Abbas, lakini nasema kwamba tumempoteza mwanazuoni mkubwa, kwa sababu mwanazuoni anapofariki, hutokea pengo na ufa katika Uislamu ambao hakuna kitu kinachoweza kuujaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha